Home Habari za michezo UKIACHA CHAMA NA BANDA…HAWA HAPA MASTAA WENGINE SIMBA WATAKAOKOSEKANA LEO DHIDI YA...

UKIACHA CHAMA NA BANDA…HAWA HAPA MASTAA WENGINE SIMBA WATAKAOKOSEKANA LEO DHIDI YA IHEFU..

MASTAA waliofunga jumla ya mabao matano ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda yatakosekana leo Uwanja wa Mkapa kutokana na sababu mbalimbali.

Timu hiyo ambayo imetoka kuonja joto ya kupata pointi moja ugenini baada ya ubao wa Uwanja wa Liti kusoma Singida Big Stars 1-1 Simba leo ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Ihefu.

Nyota sita wanatarajia kuukosa mchezo huo ikiwa ni Peter Banda ambaye katupia bao moja ndani ya ligi akiwa amecheza mechi tano huyu alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars.

Clatous Chama katupia bao moja ndani ya ligi na pasi tatu za mabao akiwa amecheza mechi 8 na kuyeyusha dakika 712 anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu na Kamati ya Uendeshaji wa ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania.

Augustino Okra amecheza mechi 8 kayeyusha dakika 439 katupia mabao matatu, Nelson Okwa amecheza mechi mbili kayeyusha dakika 13, Jimsone Mwanuke hajacheza mchezo wowote wa ligi na Israel Mwenda amecheza mechi tatu na kuyeyusha dakika 202 hawa bado hawajawa fiti.

Mgunda amesema kuwa kila mchezaji anapokosekana kuna kazi ya kuanza mpango upya.

“Mchezaji yoyote wa Simba ni muhimu na pale anapokosekana mpango kazi unakuwa umevurugwa lakini tuna jukumu la kuwaombea hawa wachezaji wetu ili wawe salama waendelee na majukumu yao,” alisema Mgunda.

SOMA NA HII  KAPOMBE:- TULIFURAHIA KUPANGWA NA WASAUZI..LAZIMA TULIPIZE KISASI CHA MWAKA JANA...