Home Habari za michezo SIMBA YAPATA DAWA MPYA….OKRAH NDANI…IHEFU WAPANIA KUPIGA KWENYE MSHONO…

SIMBA YAPATA DAWA MPYA….OKRAH NDANI…IHEFU WAPANIA KUPIGA KWENYE MSHONO…

Habari za Simba

KOCHA wa Simba, Juma Mgunda amesema upungufu ulioonekana kwenye mechi iliyopita dhidi ya Singida Big Stars (SBS) baada ya kuwakosa, Clatous Chama na Augustine Okrah hautakuwepo kwenye mechi ya leo Jumamosi dhidi ya Ihefu FC ambayo inashika mkia huku ikitamba kufanya maajabu Dar.

Mechi hiyo inachezwa saa 1:00 usiku ambapo Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 na SBS huku vibonde Ihefu wakipigwa bao 1-0 na Azam FC.

Mgunda alisema kutokuwepo kwa Chama kulileta upungufu hasa wakati wa kushambulia na lakini habari nzuri kwa timu kuna urejeo wa Okrah.

“Uwepo wa mchezaji kama Okrah kwenye kikosi na ubora wake alionao wakati huu naamini kuna uimara ataongezeka ndani ya timu yetu tofauti na mchezo uliopita,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Kwenye mazoezi ya siku mbili baada ya kurejea kutoka Singida kuna vitu vya kiufundi tumevifanyia kazi kama silaha kwetu na tumewapatia wachezaji wengine ili kwenda kucheza kwa ubora zaidi ya wapinzani wetu,”alisema Mgunda.

Kulingana na mazoezi ya Simba kutakuwa na mabadiliko kwenye safi ya ushambuliaji tofauti na mechi iliyopita.

Safu ya ushambuliaji Simba huenda akaanza na Habibu Kyombo aliyeanzia benchi mechi ya Singida, Okrah aliyekosekana na kinara wa mabao, Moses Phiri.

Kwa upande wa kocha wa Ihefu FC, Juma Mwambusi akizungumzia kikosi chake alisema anawaheshimu Simba kutokana na ukubwa wa timu yao na kuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu lakini anaamini katika dakika 90 za mchezo hana hofu.

“Tumeiandaa timu kushindana na tayari tumefika kuipigania ili tuweze kupata matokeo na kujiimarisha zaidi kwaajili ya kutetea kushuka tulipotoka,” alisema Mwambusi ambaye kikosi chake kimesheheni mastaa wazoefu hususani kwenye viwanja vya Dar es Salaam.

Mwambusi ambaye ni kocha wa zamani wa Mbeya City, Yanga na Azam naye hataingia kinyonge uwanjani kwania anawategemea mastaa wake kama Nico Wadada, Never Tigere, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Joseph Mahundi ambao wanaweza kufanya chochote kutokana na ukongwe wao.

SOMA NA HII  WADAU WA SOKA LA BONGO WATAKA KOCHA MPYA WA SIMBA APIMWE HIVI