Home Habari za michezo YACOUBA : NAISUBIRI YANGA TU….SINA CHA KUPOTEZA…

YACOUBA : NAISUBIRI YANGA TU….SINA CHA KUPOTEZA…

Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Songne amesema kwasasa yuko sawa na kwamba anasubiri maamuzi ya mabosi wa klabu yake juu ya kurejea kundini kufuatia kuondolewa katika usajili wa msimu huu.

“Kwa sasa niko sawa kabisa namshukuru Mungu nimekuwa katika matibabu, nitarejea uwanjani kucheza wakati wowote,” alisema Yacouba.

“Nawashukuru mashabiki wote, viongozi na madaktari ambao walisimamia matibabu yangu, mashabiki wasubiri muda si mrefu wataniona tena uwanjani.

DAKTARI HUYU HAPA.

Daktari aliyesimamia matibabu ya mshambuliaji huyo, Youssef Mohamed alisema kwa sasa raia huyo wa Burkina Faso yuko sawasawa baada ya kupona vizuri na hata kufanya mazoezi ya kutosha.

Youssef alisema walikuwa katika mapambano makubwa kusimamia matibabu ya mshambuliaji huyo kutokana na bado alikuwa ni mchezaji mwenye ubora mkubwa kurejea tena uwanjani.

“Hii hatua ambayo amebakiza sasa ni mambo ya kiutawala lakini Yacouba alishapona muda mrefu na alichokuwa anafanya ni kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili,” alisema Youssef raia wa Tunisia.

“Tuliamini kwamba ni mchezaji ambaye kwa umri wake bado anaweza kuja kuwa na mchango mkubwa na hata majeraha yake yaliluwa yanatibika, niwashukuru sana viongozi wa Yanga na wadhamini wetu, GSM kwa jinsi walivyopambana naye, hii ilikuwa ni hatua ya ukomavu wao mkubwa.”

SOMA NA HII  BALEKE HUYOOO JANGWANI, ISHU KAMILI IKO HIVI YANGA WANABALAA