Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA KUWATANDIKA BAKORA TZ PRISONS JANA….YANGA WAIFUATA NAMUNGO ‘ASUBUHI ASUBUHI’…

admin December 5, 2022 9:04 am

MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga umesafiri saa 11:00 alfajiri ya leo kuelekea mkoani Lindi, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo.

Kwa kutumia shirika la ndege la Precision, msafara huo utatua uwanja wa ndege wa Mtwara kisha kuunga kwa basi kuelekea Ruangwa, Lindi.

Wachezaji walioambatana na timu ni pamoja na Djigui Diarra, David Bryson, Erick Johola, Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Djuma Shabani, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Jesus Moloko, Tuisila Kisinda, Denis Nkane, Clement Mzize, Aziz Ki, Bernard Morrison, Fiston Mayele, Dickson Ambundo na Feisal Salum.

Kiungo Salum Abubakari na winga Farid Mussa watakosekana kwenye mchezo huo kwa sababu ya majeraha.

A-Z YA JINSI FEI TOTO ALVYOPELEKA MAAFA TZ PRISONS NA SIMBA JANA… BREAKING NEWS:…MKWASA ATEMANA NA KINA MASAU BWIRE…CHANZO HIKI HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply