Geita Gold FC

BAADA YA KUULILIA SANA ‘WEMBE’…NDOA YA GEITA GOLD NA MPOLE YAVUNJIKA RASMI…

admin December 7, 2022 7:50 pm

Klabu ya Geita Gold yenye maskani yake Mkoani Geita, imeachana na mshambuliaji wake George Mpole.

Geita Gold haikuweka wazi sababu hasa za kuvunja Mkataba na mpachika nyavu huyo aliechukua kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2021/2022 akimpiku Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele.

George Mpole alikuwa na mvutano na mabosi wa Geita Gold kwa miezi kadhaa huku akijitenga na timu kwa kile alichodai kuwa ni mgonjwa lakini pia anadai maslahi yake.

Mara kadhaa uongozi wa Geita Gold ulikanusha hadharani madai ya mchezaji huyo na hatimaye sasa ndoa ya wawili hao imefika tamati.

Kwa sasa Mpole yuko huru kujiunga na klabu yoyote.

KUHUSU USAJILI MPYA DIRISHA DOGO…SIMBA WATOA TAMKO RASMI…MFUMO UTAKAOTUMIKA NI HUU HAPA… AHMED ALLY APIGILIA MSUMARI DILI LA NTIBAZONKIZA KUTUA SIMBA…AGUSIA ISHU YAKE NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply