Home Habari za michezo WALIOPIGWA GOLI 9-0 NA AZAM FC…WAIBUKANA HAYA MAPYA…WAMTAJA MANDONGA….

WALIOPIGWA GOLI 9-0 NA AZAM FC…WAIBUKANA HAYA MAPYA…WAMTAJA MANDONGA….

Tangu kuanzishwa Mkoa wa Katavi haujawahi kuwa na timu yoyote ya First League, Championship wala Ligi Kuu na sasa Malimao FC imepania kufanya kweli na kumaliza kiu ya wadau na mashabiki kuzipeleka Simba na Yanga mkoani humo.

Katavi ilianzishwa rasmi Machi 1, 2012 ikiwa na mikoa mingine mitano, Njombe, Geita, Songwe na Simiyu lakini haijawahi kuziona Simba na Yanga, jambo linalowaumiza wadau na mashabiki mkoani humo.

Katibu Mkuu wa Malimao FC, John Mwanjali alisema baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la shirikisho (ASFC) kwa sasa wamehamishia nguvu kwenye maandalizi ya ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) kusaka tiketi ya first league. Alisema kinachowapa matumaini ni namna ambavyo kipigo cha mabao 9-0 dhidi ya Azam kilivyowapa umaarufu mkoani Katavi na wadau wa soka na mashabiki wamewatia moyo.

“Sisi kama Mandonga, tukipigwa kama tumepiga, kipigo hicho kimetupa umaarufu sana na ndio maana tunatumia nafasi hiyo kusaka wadau kutuunga mkono ili kujiweka fiti na RCL,” alisema Mwanjali.

Aliongeza baada ya mechi yao na Azam timu haijavunja kambi na wanaendelea na mazoezi chini ya kocha mkuu, Said Manga kuhakikisha upungufu uliojitokeza kiufundi unafanyiwa kazi.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Manga alisema ili kuhakikisha wanafikia malengo anatarajia kuongeza nguvu ya wachezaji wasiopungua wanane ili michuano itakapoanza wawe fiti zaidi.

“Tunaendelea na mazoezi kusahihisha yale makosa tuliyoona, bado sijafikiria kuacha mchezaji yeyote isipokuwa tutaongeza kama wanane, lengo ni kuona Malimao tunapanda daraja,” alisema.

Katibu mkuu wa chama cha soka mkoani humo, (KRFA) Benard Gama, alisema kutokana na mwenendo wa timu hiyo, imewaamsha kuhakikisha wanaisapoti timu hiyo, huku akieleza bado mwamko wa wadau ni mdogo.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUPOTEANA JANA...MABOSI YANGA SC WAMAUA KUFANYA KUFRU MECHI NA WANIGERIA...