Habari za michezo

RONALDO KUJIUNGA NA WARABU KWA DAU LA TRILIONI 1…

admin December 21, 2022 1:01 pm

Taarifa kutoka nchini Hispania zinaripoti kuwa mchezaji bora wa dunia mara tano (5) Cristiano Ronaldo anatarajia kusaini mkataba wa miaka 2 na nusu na klabu ya Al Nassr ya Saudia Arabia mwishoni mwa mwaka huu, mkataba utakaomalizika Juni 2025.

Thamani ya mkataba huo inatajwa kuwa ni Euro millioni 200 kwa msimu, hivyo mpaka utakapomalizika inatarajiwa kufikia Euro milioni 500 ambayo ni zaidi ya Trioni 1, bilioni 238 na milioni 178 kwa pesa ya Tanzania.

Ronaldo (37) raia wa Ureno, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Manchester United kwa makubaliano ya pande zote mbili. Kwa upande mwingine imekuwa ikiripotiwa kuwa bado anataka kuendelea kucheza soka barani Ulaya.

USAJILI MPYA YANGA SC UHAKIKA…KABWILI ATAJWA TENA… WAKATI SIMBA WAKIFANYA SIRI…GEITA GOLD WAMNG’ANG’ANIA SAIDO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply