Geita Gold FC

WAKATI SIMBA WAKIFANYA SIRI…GEITA GOLD WAMNG’ANG’ANIA SAIDO..

admin December 21, 2022 1:08 pm

Kuelekea mchezo kati ya Wenyeji Geita Gold FC Azam FC Matajiri wa Chamazi, Kocha Msaidizi wa Geita Gold Mathias Wandiba amefunguka na kusema mchezaji Saido Ntibazonkiza bado mchezaji wao.

Akizungumza na Waandishi wa habari Wandiba amekanusha taarifa za kuondoka kwa Nyota huyo wa Burundi na kusema bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo huku akiwataka mashabiki kuhudhuria mchezo wao na Azam kesho.

“Kikubwa suala Saidoo sio jukumu langu sana kulizungumzia mimi mpaka sasa hivi ni kama mwalimu na bado nategemea kwamba ni mchezaji wetu kwa sababu hatujapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi iliyokamilika”

RONALDO KUJIUNGA NA WARABU KWA DAU LA TRILIONI 1… MASIKINI TAMBWE WEEH… YAMKUTA YA KUKUMKUTA NA SINGIDA BIG STARS…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply