Yanga SC kusajili mastaa Azam FC
Azam FC

YANGA SC WAJIBU MASHAMBULIZI AZAM FC…WAPANIA KUBEBA AKAMINKO NA KIPRE JR…

admin December 29, 2022 7:20 am

Vita ni vita baina ya vigogo wawili. Klabu ya Yanga SC imetuma maombi rasmi hii leo kwenda klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuwasajili kiungo James Akaminko pamoja na Kipre Jr.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa za Kiungo nyota wa Yanga SC, Feisal Salum kuvunja mkatana wake na Yanga akitajwa kutaka kutimkia Azam FC.

Uongozi wa Azam  kupitia kwa Kaimu Afisa Habari wake, Hasheem Ibwe umekiri kupokea maombi ya Yanga SC na kueleza kuwa bado kuna taratibu zinaendelea kufuatwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ibwe ameandika;

“Azam fc inathibitisha kupokea Maombi Ya Yanga  mapema leo juu ya uwezekano wa kunasa saini ya nyota wetu wawili JAMES AKAMINKO na KIPRE JUNIOR.

Maombi yamepokelewa na hivi karibuni watajibiwa kama wanapatikana au la! Na hiyo ni Baada ya Vikao vya ndani kufanyika pande zote 2″.

KISA FEI TOTO KUHUSISHWA NA AZAM FC….YANGA SC WAPANGA KUSUSIA BIDHAA ZA AZAM… HII KWA WAJANJA TU…TUMIA BURSTING HOT 5 YA MERIDIANBET KWA UHAKIKA WA MKWANJA…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply