Home Habari za michezo JINA LA MAYELE LAZIDI KUTIKISA AFRIKA…AWEKWA KAPU MOJA NA NABY KEITA WA...

JINA LA MAYELE LAZIDI KUTIKISA AFRIKA…AWEKWA KAPU MOJA NA NABY KEITA WA LIVERPOOL…

Habari za Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele, amekuwa miongoni mwa wachezaji bora katika kikosi cha mwaka 2022, kwa mujibu wa mtandao wa Foot-Afrika kutokana na ubora, kiwango chake ambacho amekuwa akionyesha na miamba hiyo.

Mayele ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara hadi sasa akifunga 14 na kuifukuzia rekodi yake ya mabao 16 aliyofunga msimu uliopita nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole aliyemaliza kinara na 17.

Katika kikosi cha kwanza kilichotolewa kinaundwa na Yassine Bounou (Morocco/ Sevilla FC) ambaye anakumbukwa zaidi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomaliza Qatar kutokana na kuisaidia timu yake kuishia hatua ya nusu fainali.

Kwa mwaka 2022 Bounou alicheza michezo 56 na kutoruhusu bao (Assisti) mechi 17 kwenye mashindano yote akiwa ni mchezaji bora mara saba huku akiingia pia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kipa bora wa Dunia.

Mbali na Bounou wachezaji wengine ni Achraf Hakimi (Morocco/ PSG), Chancel Mbemba (DRC/ Marseille), Kalidou Koulibaly (Senegal/ Chelsea), Andre Zambo-Anguissa (Cameroon/ Napoli), Sofyan Amrabat anayechezea Morocco na Fiorentina.

Nyota wengine ni Sadio Mane (Senegal/ Bayern Munich), Riyad Mahrez (Algeria/ Manchester City), Vincent Aboubakar (Cameroon/ Al-Nassr), Mohamed Salah (Egypt/ Liverpool) na Victor Osimhen wa Nigeria na Napoli.

Kikosi cha pili ambacho anapatikana Mayele kina mastaa kama Edouard Mendy (Senegal/ Chelsea), Edmond Tapsoba (Burkina Faso/ Bayer Leverkusen), Ramy Bensebaini (Algeria/ Borussia Monchengladbach) na Mohamed Camara wa (Mali / AS Monaco).

Wengine ni Aissa Laidouni (Tunisia/ Ferencváros), Ismael Bennacer (Algeria / AC Milan), Seko Fofana (Ivory Coast / RC Lens), Naby Keita (Guinea / Liverpool), Fiston Mayele (DRC/ Yanga), Eric Choupo-Moting (Cameroon/ Bayern Munich) na mshambuliaji wa timu ya taifa wa Ivory Coast na Borussia Dortmund, Sebastien Haller.

SOMA NA HII  KISA DJUMA...NABI AKIRI KUPATWA 'KIZUNGUZUNGU' YANGA...AFUNGUKA NAMNA ANAVYOWEWESEKA NAYE...