Home Habari za michezo AHMED ALLY: ‘UNBEATEN’ YA YANGA ILIKUWA NI MATUSI KWA SOKA LA NCHI…

AHMED ALLY: ‘UNBEATEN’ YA YANGA ILIKUWA NI MATUSI KWA SOKA LA NCHI…

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaponda wapinzani wao Yanga baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Klabu ya Ihefu FC yenye makazi yake Mbalali Mkoani Mbeya.

“Unbeaten yenu ilijaa magoli mengi ya offside na Penati za gubu la wifi. Hata jana tayari mlishatengeneza unbeaten ya offside, mfungaji wenu alikua kasimama mbele peke yake kama dereva wa treni.

“Waamuzi zaidi ya wanne wamefungiwa wakiwasaidia kutengeneza unbeaten na mwingine mmoja ameshtakiwa kamati ya waamuzi tunasubiri hukumu. Sisi tunaheshimu ubora wa wapinzani lakini hatuheshimu unbeaten ya mchongo kama yenu.

“Nyie kuendelea kuwa unbeaten ilikua ni kuutukanisha mpira kwa sababu hamna hiyo quality. Niko palee nakula mihogo Kama una makasiriko nawe agiza mihogo na bofya link hii katazame timu yenye quality Bora mnyama Simba SC,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SENZO AFUNGUKA MAPYA KUHUSU USAJILI WA MORRISON YANGA NA KUONDOKOKA KWAKE..."UONGO HUPEWA SANA NAFASI TZ"...