Home Habari za michezo PAMOJA NA KUFUNGWA NA IHEFU JUZI…YANGA KUFANYA ‘BONGE LA PARTY’ KUSHEREKEA ‘UNBEATEN’…

PAMOJA NA KUFUNGWA NA IHEFU JUZI…YANGA KUFANYA ‘BONGE LA PARTY’ KUSHEREKEA ‘UNBEATEN’…

Yanga SC, inatarajia kufanya bonge moja la pati la kusherehekea kucheza mechi 49 bila kupoteza (unbeaten).

Afisa habari wa Yanga, Ally Kamwe ameyasema hayo leo Desemba Mosi, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM kuelekekea mchezo wao wa Jumapili (Desemba 4) dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Tunakwenda kufanya bonge la pati, yale mliokuwa mnaona sijui ya kusimama uwanjani, kula keki zile zilikuwa ni amsha amsha, shughuli yenyewe inakwenda kufanyika Jumapipi.

“Tutakuwa na orodha ndefu sana ya wasanii, mashabiki na wanachama wa Yanga siku hiyo watapata nafasi ya kupiga picha kuna sehemu maalum ya kupiga picha na kufanya mahojiano kwa mashabiki wetu na tumealika vyombo vya habari kutoka nje kuja kuripoti tukio hili la kihistoria,” alisema Kamwe.

Yanga inashuka dimbani Jumapili kuwavaa Tanzania Prisons ikiwa ni baada ya kupokea kichapo cha 2-0 kutoka kwa Ihefu FC ambao ndio waliitibulia Yanga sherehe za kuendelea kuhesabu unbeaten.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI