Home Habari za michezo PAMOJA NA IHEFU KUWASAIDIA JUZI…SIMBA WAENDELEA KUWEWESEKA NA YANGA…

PAMOJA NA IHEFU KUWASAIDIA JUZI…SIMBA WAENDELEA KUWEWESEKA NA YANGA…

Habari za Simba SC

Yanga ipo kileleni mwa amsimamo wa Ligi Kuu Bara na ilikuwa na pointi 32 ikiwa nyuma michezo miwili kumaliza raundi ya kwanza inayotakiwa zichezwe mechi 15, huku Simba ikiwa na mchezo mmoja.

Yanga kabla ya mchezo dhidi ya Ihefu ilikuwa imefikisha michezo 49 bila kufungwa, ambapo hadi sasa msimu huu ina sare mbili, Simba mechi 13 ina sare nne, imefungwa mmoja dhidi ya Azam na imeshinda tisa na hilo linaipa presha kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa.

Endapo Simba ikishinda mechi moja iliyobaki ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Desemba 3 itakuwa na pointi 34 na kama Yanga ikishinda zote itakuwa na pointi 41, hivyo zitakuwa zimepishana pointi saba.

Japokuwa safu ya ushambuliaji ya Simba imetengeneza idadi kubwa ya mabao 28 na kutikiswa mara saba nyavuni, wakati Yanga kutegemeana na mchezo dhidi ya Ihefu jana, lakini ilikuwa inamiliki mabao 23 na imetikiswa mara sita nyavuni.

Nahodha wa Simba, John Bocco ambaye anamiliki mabao manne aliwahi kukaririwa akisema wanaendelea kupambana na kwamba imesalia michezo mingi itakayoamua ubingwa. “Tupo kwa ajili ya kuisaidia timu kufikia malengo yake kabla ya kutanguliza maslahi binafsi,” alisema, huku straika mwenzake, Moses Phiri akisema wanapambana kila mechi wapate mabao mengi: “Hakuna ligi rahisi tunahitaji kusimama kwenye malengo ya klabu ambayo ni ubingwa.”

Straika wa Yanga, Fiston Mayele ambaye ni kinara wa mabao alikaririwa akisema: “Nikipata nafasi ya kufunga nitafunga sana, ila jambo la msingi ni kuipambania Yanga ili kuendeleza kutokufungwa pia kuutetea ubingwa.”

SOMA NA HII  BAADA YA WACHAMBUZI KUSEMA SANA...HATIMAYE SIMBA WAAMUA KUMRUDISHA KUNDINI DILUNGA KWA STAILI HII...