Home Azam FC BAADA YA MASHABIKI YANGA KULIANZISHA…AZAM FC WAMKANA FEI TOTO..

BAADA YA MASHABIKI YANGA KULIANZISHA…AZAM FC WAMKANA FEI TOTO..

Tetesi za Usajili Yanga

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkareem Amin ‘Popat’ amesema klabu yao haina mpango wowote wa kumsajili Kiungo wa Yanga FC Feisal ‘Fei Toto’.

Kiungo huyo amekua gumzo katika vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii, kufuatia taarifa aliyoiweka katika Ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram mwishoni mwa juma lililopita, akiwaaga Mashabiki, Wanachama na Wachezaji wenzake wa Young Africans na baadae Uongozi kumjibu.

Popat amekanusha taarifa za kuwaniwa kwa Kiungo huyo alipohojiwa na Kituo cha Radio cha Wasafi FM mapema leo Alhamis (Desemba 29), ambapo amesema wanaona na kusikia Klabu yao inatajwa kwenye sakata la Mchezaji huyo, lakini hawana mpango wowote wa kumsajili.

Popat amesema Azam FC inafahamu utaratibu wa kumsajili mchezaji mwenye mkataba na asiye na Mkataba na mara zote imekua inafuata utaratibu wa kikanuni, hivyo inawashangaza sana kuona Klabu yao inaingizwa kwenye Sakata la ‘Fei Toto’.

“Sisi wenyewe tunasoma tu mitandaoni kuhusu Feisal Salum. Hakuna siku tuliyowahi kukaa na kusema tunamtaka Feisal. Yule ni mchezaji mzuri na tegemeo katika timu yake ya Yanga na timu ya taifa.”

“Hakuna timu ambayo haiwezi kumtamani Feisal, lakini sisi kama Azam FC hatuna taarifa ya namna hii maana hakuna sehemu tuliyosema wala kuandika kuwa tunamtaka Feisal “

“Halafu Azam FC tunafahamu namna ya kumsajili Mchezaji mwenye Mkataba na Klabu yake na tumefanya hivyo mara kadhaa, Pia tunajuwa namna ya kumsajili mchezaji ambaye hana Mkataba yaani yupo huru, kwa sasa nini ionekane tunaharibu heshima yetu kwa huyo anayetajwa?” amehoji Popat.

Jana , Viongozi wa matawi ya Yanga SC kwa umoja wao waliibuka mbele ya waandishi wa habari na kuipiga mkwara Azam, kuwa kama wanahusika na kumsajili Fei Toto basi wangesusia kununua bidhaa za kampuni hiyo.

Hata hivyo, kauli hio haijapata nguvu ya kuungwa mkono na viongozi wakuu wa Yanga SC, kwani ukizingatia kuwa Timu hiyo na Kampuni inayoisimamia Azam FC wanamikataba mingi ya kibiashara baina ya pande mbili.

SOMA NA HII  HAWA AZAM FC MSIMUU HUU HAWATAKI 'MBOMBELA' AISEE...WAIFUATA MBEYA CITY NA 'UGWADU' KAMA WOTE...