Home Habari za michezo KISA FEI TOTO KUHUSISHWA NA AZAM FC….YANGA SC WAPANGA KUSUSIA BIDHAA ZA...

KISA FEI TOTO KUHUSISHWA NA AZAM FC….YANGA SC WAPANGA KUSUSIA BIDHAA ZA AZAM…

Habari za Yanga

Vita ya chuki ni kama imechukua nafasi hivi baada ya sakata la kiungo wa Yanga SC Feisal Salum kutaka kuvunja Mkataba na kutimkia Azam FC.

Wakati sakata hilo likiwa bado linaendelea kufukuta wazee wa Yanga na viongozi wa Matawi wamekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia skata hilo.

Kitendo cha Feisal kutaka kuondoka Yanga SC na kutajwa kujiunga na Azam FC ni kama kimeibua chuki kwani wametoa azimio zito kuelekea kwa Kampuni ya Azam na bidhaa zake

” Kama Viongozi wa Yanga wakibaini Azam FC ndio wanamdanganya Feisal Salum aende kwao basi tunawaomba Viongozi wetu wavunje ule mkataba wetu na Azam halafu na sisi mashabiki wa Yanga SC hatutanunua bidhaa zozote za Azam ” wamesisitiza wazee hao.

Tukio hilo la aina yake linakuja ikiwa zimepita siku kadhaa toka Fei Toto kuanika wazi msimamo wake wa kuvunja mkataba na Yanga , ambapo hata hivyo mabosi wa Jangwani walitumia watu mbali mbali wenye ushawishi kumtaka abatilishe uamuzi huo lakini alikataa.

Hata hivyo, inaelekeweka wazi msimamo huo ni ngumu kutekelezeka haswa ukizingatia bidhaa za Azam zimekuw sehemu muhimu ya maisha ya mtanzania wa kawaida.

Aidha, msimamo huo wa mashabiki wa Yanga , unaweza pia ukawa na mwitikio chanya kama viongozi wa Yanga wakiupitisha na kuufanya kuwa wa klabu kwa ujumla.

Hata hivyo, jambo hilo ni gumu kutokea, kwani Yanga wamekuwa ni sehemu ya wanufaika wa kampuni la Bakhresa ambao ni wamiliki wa bidhaa za Azam, ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya Azam FC.

Kwa miaka ya hivi karibuni inasemekana pia, Yanga walihusika kumchochea aliyekuwa kiungo wa Azam FC , Salum Abubakari, maarufu kama Sure Boy kuachana na timu hiyo ili ajiunge nao jambo ambalo lilifanikiwa.

Katika sakata hilo, Azam FC wala mashabiki wake wa soka hawakujitokeza mbele ya kamera za waandishi wa habari kuhusisha sakata hilo na klabu ya Yanga.

Hii si mara moja kwa klabu kubwa za Tanzania kuchukuliana wachezaji, aidha kwa njia hiyo au ya kungojea mikataba iishe, kwani miaka mitano nyuma Simba waliwasajili wachezaji wanne wa Azam FC mara baada ya mikataba yao kuisha Chamazi.

Wachezaji hao ni pamoja na Aishi Manula, John Bocco, Gardiel Michael pamoja na Erasto Nyoni.

 

SOMA NA HII  MSHERY 'KUPIGWA KISU' TUNISIA...YANGA WAAMUA LIWALO NA LIWE...ISHU NZIMA IKO HIVI...