Home Habari za michezo LICHA YA KUIBUKA NA GOLI 5 …HIZI HAPA REKODI ZA KIBABE ZILIZOWEKWA...

LICHA YA KUIBUKA NA GOLI 5 …HIZI HAPA REKODI ZA KIBABE ZILIZOWEKWA NA SIMBA JANA..

Habari za Simba

MVUA ya mabao 5-0 imewanyeshea wachimba madini, Geita Gold wakiwa nyumbani dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Simba kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza yalifungwa na Pape Sakho mara mbili, Kibu Dennis, Clatous Chama na John Bocco.

Ushindi huo mnono, umewafanya vijana wa Juma Mgunda kufikisha jumla ya pointi 37, wameachwa kwa pointi nne na Yanga yenye pointi 41 ikiwa kileleni.

Huu ni ushindi mkubwa zaidi kwa Simba kupata kupata dhidi ya Geita Gold, ndani ya michezo miwili ambayo amekutana kwenye Ligi yamefungwa mabao manane huku wachimba madini hao wakiwa hawajafunga hata moja.

Hakuna mchezo ambao Simba imepoteza msimu huu kwenye michuano yote ikiwa winga wake amepachika bao kwenye mchezo huo.

Mabao mawili ambayo Sakho amefunga dhidi ya Geita Gold, yamemfanya winga huyo wa kimataifa wa Senegal kufikisha mabao matano kwenye ligi.

Mvua ya mabao matano ambayo Geita Gold imekumbana nayo imewafanya kushuka kwa nafasi moja kwenye msimamo wa ligi kutoka ya sita hadi saba.

Hiki ni kipigo kikubwa zaidi kwa Geita Gold kukumbana nacho kwenye ligi tangu kupanda kwao daraja.

Mbali na bao kideo ambalo Chama alifunga alitoa lakini pia alifikisha asisti yake ya tisa msimu huu baada ya kutoa mbili kwenye mchezo huo ambao alipiga mashuti mawili yaliyolenga lango.

Chuma cha tano ambacho alipachika Kibu kwenye mchezo huo, lilikuwa bao lake la kwanza msimu huu.

SOMA NA HII  YANGA WATUA NIGERIA,MATIZI KUPIGA LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here