Home Habari za michezo MIL 350 KUMSHUSHA PACHA WA PHIRI SIMBA SC….JAMAA LINAJUA HILOO…

MIL 350 KUMSHUSHA PACHA WA PHIRI SIMBA SC….JAMAA LINAJUA HILOO…

SIMBA SC inatakiwa ivunje benki na kutenga kitita cha Sh 350Mil ili kufanikisha usajili wa straika wa Power Dynamo ya nchini Zambia, Kennedy Musonda ili kuwa pacha wa Mzambia mwenzake, Moses Phiri kikosini hapo.

Zambia wanatokea wachezaji wawili tegemeo hivi sasa katika kikosi cha Simba SC ambao ni kiungo Clatous Chama na Moses Phiri anayecheza nafasi ya ushambuliaji kama ilivyo kwa Musonda.

Simba SC hivi sasa ipo katika mipango ya kukiboresha kikosi chake ili kifanye vema katika michuano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika wakitinga hatua ya makundi.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, kimesema kwamba, katika kusaka mshambuliaji, wameweka mitego kwa nyota wawili, wakimkosa Cesar Manzoki anayekipiga Dalian Proffessionalya nchini China, basi wataangukia kwa Musonda.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kwamba, Musonda amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani hiyo ya dau la usajili baada ya klabu yake kukubali kumuachia.

“Mazungumzo na wakala wa Musonda yanakwenda vizuri, kutazama namna ya kukamilisha dili la usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Zambia anayeichezea Power Dynamos.

“Musonda ni kati ya washambuliaji wanaofanya vizuri hivi sasa ligi ya huko nyumbani kwao, hivyo uongozi unaamini ni mbadala mzuri wa Manzoki kama akikosekana yeye,” kilisema chanzo hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ alizungumzia hilo la usajili na kusema: “Tumepanga kufanya usajili kufuatia ripoti ya kocha wetu Mgunda (Juma), kikubwa Wanasimba wawe watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi unaingia sokoni kufanya usajili.”

SOMA NA HII  JAMA JAMA..HAWA WAANGOLA WAMEPANIA AISEE...'CHEKI' MPUNGA WATAKAO PEWA WACHEZAJI WAO WAKISHINDA KESHO..