Home Habari za michezo MKAKATI WA SIMBA KWA LIGI KUU TZ UKO HIVI….KAZI KUANZA RASMI KESHO….

MKAKATI WA SIMBA KWA LIGI KUU TZ UKO HIVI….KAZI KUANZA RASMI KESHO….

Habari za Simba

Kikosi cha Simba kina kazi ya kusaka ushindi Desemba 18,2022 Uwanja wa CCM Kirumba mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa mzunguko wa pili kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda.

Mapema jana Desemba 16 kikosi hicho kiliwasili Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa ligi.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilipata ushindi wa mabao 3-0 na kusepa na pointi zote tatu.

Mgunda amesema kuwa wanatambua mechi ni ngumu na kila timu inahitaji ushindi hivyo watapambana kupata ushindi.

“Wapinzani wetu wanapambana kupata matokeo nasi tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi ambacho tunakifanya ni kila mmoja kutimiza majukumu yake.

“Mashabiki wawe pamoja nasi kwa kuwa mashabiki ninawaita wachezaji wetu wa 12 wamekuwa wakiongeza nguvu kwenye mapambano yetu,” Mgunda amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara wa Simba ni pamoja na John Bocco, Kibu Dennis,Moses Phiri,Sadio Kanoute na Henock Inonga.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII MPYA...KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA