Home Habari za michezo SIMBA SC WAMPANIA DICKSON JOB…WAMWEKEA MIL 200 NA MSHAHARA WA MIL 10…

SIMBA SC WAMPANIA DICKSON JOB…WAMWEKEA MIL 200 NA MSHAHARA WA MIL 10…

Habari za Yanga SC

Kabla ya sekeseke la kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ halijapoa la kuvunja mkataba na timu hiyo na waajiri wake kumgomea, limeibuka lingine la beki wa kati wa timu hiyo, Dickson Job ambaye ni panga pangua kikosi cha kwanza.

Hivi karibuni baada ya kuibuka taarifa ya Fei Toto kupeleka pesa benki kwa ajili ya kuvunja mkataba na Yanga SC, jambo ambalo limezua taharuki kwa mashabiki, limeibuka la Job kutembea na mikataba ya timu mbili yenye ofa tofauti.

Chanzo cha kuaminika kinasema vigogo wa Yanga SC tangu litokee jambo la Fei Toto wameanza mchakato wa kumalizana na mastaa wengine ambao mikataba yao inaelekea mwishoni, ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na kuongeza mishahara.

Ipo hivi: Mkataba wa Job na Yanga SC unaishia mwishoni mwa msimu huu, baada ya kusaini miaka miwili msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar na chanzo kilieleza kwamba kapokea ofa nono ya Simba SC tofauti na anayopewa na waajiri wake wa sasa, jambo linalomfanya achukue muda wa kutafakari ili kufanya maamuzi sahihi asije akajuta.

“Kapokea ofa ya Simba SC inayoonekana ni shilingi 200 milioni na mshahara wa milioni 10 kwa mwezi, wakati Yanga inamuongezea mshahara hadi milioni saba kutoka tatu na dau la usajili ni milioni 70, sasa anazitafakari ofa zote mbili.

“Naona ni kama uongozi umeshtuka kwa maamuzi aliyofanya Fei Toto kwamba yanawapa nguvu wachezaji wengi kupigania wanachostahili, maana wakiliacha na hilo la Job watazidi kuwachanganya mashabiki na wanachama wa Yanga, hii mikataba yote anatembea nayo, naamini kabla dirisha dogo halijafungwa atakuwa amefanya maamuzi ya asaini wapi, yaani ni presha tupu.”

Ligi Kuu Bara ikimalizika msimu huu utakuwa msimu wa pili wa Job kukipiga Yanga na kutokana na mchango wake kwenye timu, imeelezwa anahitaji kuboreshewa maslahi yake yatakayofanya apotezee ofa ya Simba SC ambao wanaelezwa kuwa wapo siriazi sana na beki huyo wa Taifa Stars, akiwa chaguo la kwanza la kocha Nasrredine Nabi.

Ukiachana na Job, wachezaji wengine wanaotajwa mikataba yao imebakia miezi sita na Yanga haraka wanataka kuwabana ni Khalid Aucho, Jesus Moloko na kipa namba moja Djigui Diarra ambao awali waliitwa na uongozi kupewa ofa mpya lakini hawakumalizana nao.

Takwimu za Job msimu huu: amecheza mechi: 15 Dakika : 1262 Amekosa mechi :3

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA BALAA LAKE NA SIMBA....KICHUYA KAIBUKA NA HILI KWA CHASAMBI...