Home Simba SC WANNE WA SIMBA KUIKOSA POLISI TANZANIA LEO CCM KIRUMBA

WANNE WA SIMBA KUIKOSA POLISI TANZANIA LEO CCM KIRUMBA


CLATOUS Chama kinara wa utengenezaji wa pasi za mwisho ndani ya Simba akiwa nazo 13 na mabao 7 anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania.

Katika mchezo wa leo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Simba itakuwa mgeni wa Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita, Chama alipachika mabao yote mawili akitokea benchi ilikuwa zama za Sven Vandenbroeck.

Mbali na Chama pia Ibrahim Ajibu naye atakosekana kwenye mchezo wa leo kwa kuwa aliachwa Bongo kutokana na matatizo ya kifamilia sawa na Chama ambaye yupo kwao Zambia.

Wengine ni kipa namba tatu, Ally Salim naye pia anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo pamoja na Gadiel Michael ambaye ni beki wa kushoto kutokana na kutokuwa fiti kwa ajili ya mechi ya leo.

Kwa mujibu wa Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo watapambana kupata pointi tatu. 

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi  67 inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 8 na pointi 41.

SOMA NA HII  WAKATI MORRISON AKILITIBUA SIMBA....MKUDE ALIAMSHA...PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA NENO HILI...