Home news WAKATI MORRISON AKILITIBUA SIMBA….MKUDE ALIAMSHA…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA NENO HILI…

WAKATI MORRISON AKILITIBUA SIMBA….MKUDE ALIAMSHA…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA NENO HILI…


KURUDI kwa kiungo Jonas Mkude aliyekuwa majeruhi, kumempa mzuka kocha mkuu wa Simba, Pablo Franco aliyesisitiza kikosi chake kimekuwa kikibadilika kila mara kulingana na aina ya mpinzani wanayekutana naye.

Mkude pamoja na Kibu Denis walikosekana kwenye mechi tatu za mwisho za Simba kutokana na kuumia, lakini kiungo huyo mkabaji amerejea na kocha Pablo alisema ni faida kwao kwenye mechi zilizopo mbele yao.

“Kurejea kwa Mkude maana yake kuna kitu anakuja kuongeza ubora katika eneo letu la kiungo akishirikiana na wenzake anaocheza nao pamoja katika eneo hilo,” alisema Pablo na kuongeza;

“Mkude ni miongoni mwa wachezaji walio bora katika eneo hilo kutokana na uwezo wa kutimiza majukumu yake kama ilivyo kwa wengine ambao nao wanacheza katika eneo hilo.”

Kuhusu Kibu alisema; “Ni miongoni mwa wachezaji walioanza vizuri ndio maana mpaka sasa katika michezo michache aliyocheza amfunga mabao matatu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA MAGOLI YA KIZEMBE...'NDOA' YA SHIKHALO NA MTIBWA YAVUNJIKA RASMI...