Home Uncategorized MASHINE YA KAZI SIMBA YAUNGANISHWA KWENYE KIKOSI, RUKSA KUWAVAA COASTAL UNION

MASHINE YA KAZI SIMBA YAUNGANISHWA KWENYE KIKOSI, RUKSA KUWAVAA COASTAL UNION

 


BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck huenda atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Coastal Union Novemba 21, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,  Arusha.


Tayari kikosi cha Simba kimetia timu Arusha ambapo kilianza safari ya kuwafuata wapinzani wake Novemba 19 jioni na kuwasili salama jijini Arusha.


Morrison alikuwa nje kuitumikia adhabu ya mechi tatu pamoja na faini ya laki tano, (500,000) baada ya kumpiga ngumi beki wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso na wote wawili walikumbwa na adhabu hiyo iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Bara..


Nyota huyo alikosa mechi tatu ilikuwa mbele ya Mwadui FC, Kagera Sugar na ule wa dabi dhidi ya Yanga.

SOMA NA HII  YANGA YAUTAKA UBINGWA ULIOPO MIKONONI MWA SIMBA