Home Habari za michezo TAKWIMU ZINAONGEA….LOMALISA AANZA KUILIPA YANGA SC…KAZI YAKE SI YA KITOTO…

TAKWIMU ZINAONGEA….LOMALISA AANZA KUILIPA YANGA SC…KAZI YAKE SI YA KITOTO…

Lilikuwa suala la muda kwa beki wa kushoto wa Yanga SC, Joyce Lomalisa kunyamazisha kishindo cha mashabiki waliokuwa wanadhani usajili wake wamepigwa, kwani hakuanza kwa kiwango kikubwa baada ya kujiunga na timu hiyo.

Lomalisa alijunga na Yanga SC msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea Bravos do Maquis na matarajio yao yalikuwa kumuona anaingia moja kwa moja kikosi cha kwanza.

Data za Lomalisa tangu ajiunga na Yanga SC, hadi sasa amecheza mechi 13 akitumia dakika 1048 na kiwango chake kwa hivi karibuni kimekuwa msaada kwa klabu yake.

Upepo umebadilika na sasa anaonekana lulu mbele ya mashabiki wake wakifurahia shoo anayoionyesha uwanjani, huku akichangia mabao ya timu licha ya kuwa beki.

ASISTI 4

Jumla ya mabao 33 ya Yanga SC, amechangia matatu dhidi ya Singida Big Stars, alilofunga Fiston Mayele dakika ya 55, timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Asisti, nyingine alitoa dhidi ya Ihefu, bao la Yanick Bangala dakika ya tisa, Wanajangwani wakipoteza kwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting alimpa pasi ya bao Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 51, Yanga ikishinda mabao 2-1 ikiwa ugenini.

Ukiachana na Lomalisa staa mwingine, Stephane Aziz Ki akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ambaye usajili wake ndio ulitikisa zaidi kwa wageni msimu huu.

Ki hakuanza kwa kiwango walichokitarajia mashabiki ingawa walikuwa wanakiri anajua mpira kwa aina zake za pasi alizokuwa anazipiga uwanjani, ila kwa sasa naye kiwango chake kimeanza kuwa juu.

Hadi sasa Ki katika mabao 33 ya Yanga SC yaliyopatikana katika mechi 17, kachangia mabao manne kwa maana ya asisti mbili na mabao mawili.

Ki alifunga bao mojawapo kwenye ushindi wa 3-0 Yanga SC ikiichapa Mtibwa Sugar, dhidi ya Simba mpira wa kutenga timu hizo zikitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.

Asisti za mabao alitoa dhidi ya Coastal Union, mabao yaliyofungwa na Mayele dakika ya 47 na Fei Toto dakika ya 66.

Ukiachana na hao pia yupo Msongomani, Tuisila Kisinda ambaye ameanza kurejea kwenye fomu taratibu, lakini bado hajafikia kiwango chake alichokionyesha msimu 2020/21 ambapo baadaye alitimkia Morocco.

SOMA NA HII  SIMBA CHINI YA ULINZI MKALI...MABOSI WAIGOMEA GSM..KIUNGO SIMBA ATUA AZAM...