Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI:..YANGA WAIZIDI KETE SIMBA KWA BOBOSI..ASAINISHWA KININJA …ISHU NZIMA IMEFANYIKA...

TETESI ZA USAJILI:..YANGA WAIZIDI KETE SIMBA KWA BOBOSI..ASAINISHWA KININJA …ISHU NZIMA IMEFANYIKA DUBAI…

Bobosi to Yanga SC and Simba SC

Taarifa zinaeleza kuwa, Klabu ya Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, rasmi imemalizana na kiungo wa Uganda, Bobosi Byaruhanga na kumpatia mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kutua katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, mwaka huu.

Bobosi ambaye alikuwa mchezaji huru kwa muda mrefu baada ya mkataba wake na Vipers kumalizika, amekuwa akihusishwa kutakiwa na Yanga na sasa taarifa zinaeleza kuwa winga huyo amemalizana rasmi na klabu hiyo.

Chanzo chetu cha kuaminika kutoka Uganda ambacho kimeomba hifadhi ya jina lake kulingana na maslahi binafsi, kimesema kuwa, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ambaye yupo Qatar akishuhudia michuano ya Kombe la Dunia, amemalizana na kiungo huyo.

Mtoa taarifa huyo alibainisha kwamba, Injinia Hersi na Bobosi walikutana Dubai kwa ajili ya mazungumzo, kisha wakamalizana kwa kufikia muafaka wa nyota huyo kutua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Mbali na Hersi, pia uwepo wa bosi mwenyewe wa GSM, Gharib Said Mohammed huko Dubai, kumefanya dili hilo kukamilika kirahisi na haraka.

Imeelezwa kwamba, baada ya makubaliano hayo kufikiwa, Bobosi akaenda Qatar akiongozana na viongozi wa Yanga kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea.

“Ukweli upo hivyo, Bobosi kwa sasa hayupo huku Uganda, alikuwa nchini Dubai pamoja na viongozi wa Yanga, Rais wa Yanga kabla ya kwenda kuangalia mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar alipitia kwanza Dubai kwa ajili ya mazungumzo na kiungo huyo ambapo kwa sasa ambapo ninavyokueleza kila kitu kimekamilika.

“Bobosi amepewa mkataba wa miaka miwili na jambo kubwa kwa sasa ni kufahamu tu kama amekubali kuusaini au bado lakini tayari mazungumzo kati ya Bobosi na viongozi wa Yanga yamefanyika huko Dubai kabla ya viongozi hao kwenda naye Qatar,” kilisema chanzo hicho.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alizungumzia juu ya ishu ya Bobosi kujiunga na Yanga ambapo alisema: “Bobosi ni mchezaji mzuri na Yanga ni sehemu ya wachezaji wazuri kucheza, yeye mwenyewe anapenda kuichezea Yanga, hivyo tunafurahi kuona mchezaji mzuri kama yeye kuipenda timu yetu.”

SOMA NA HII  JK AFUNGUKA MAHABA YAKE KWA YANGA..AWAPA KAZI YA KUFANYA DHIDI YA SIMBA