Home Habari za michezo USAJILI MPYA YANGA SC UHAKIKA…KABWILI ATAJWA TENA…

USAJILI MPYA YANGA SC UHAKIKA…KABWILI ATAJWA TENA…

Yanga SC wanatarajia kufanya usajili wa wachezaji wawili katika dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa kuanzia Desemba 15, 2022 hadi Januari 15, 2023 kwa ajili ya kuongeza nguvu katika maeneo muhimu baada ya ushauri wa Benchi la Ufundi la timu hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said amesema watafanya usajili wa wachezaji hao kwa ajili ya maslahi makubwa ya Klabu hiyo ambayo kwa sasa imekuwa na Kikosi bora, amesema watafanya usajili huo kuboresha zaidi Kikosi chao.

“Katika dirisha hili la usajili tutafanya usajili wa Wachezaji wawili au mmoja kulingana na mahitaji ya Benchi la Ufundi ili kuongeza nguvu katika Kikosi chetu, lakini kwenye Kikosi kuna baadhi ya Wachezaji wanahitajika kwa mkopo kwa baadhi ya timu, tayari tumepokea maombi ya sajili hizo (Loan Agreement)”, amesema Mhandisi Hersi.

Mhandisi Hersi amesema Wachezaji Lazarus Kambole na Yacouba Sogne ambao walikuwa nje ya Kikosi, kwa sasa inategemea na ushauri wa Kocha na Benchi la Ufundi, kuwatumia Wachezaji hao, amesema Yanga SC ina jumla ya Wachezaji 12 wa kigeni, hivyo ili kuwaingiza Wachezaji hao wawili itabidi kuachwa Wachezaji wengine wawili waliopo Kikosini kwa sasa.

Hata hivyo, Hersi amesema kwenye Kikosi chao kuna ushindani wa hali ya juu kwa Wachezaji hao kupata nafasi ya kuingia na wengine kutoka ili kuboresha Kikosi bora chenye ushindani katika mashindano ya ndani na mashindano ya Kimataifa yaani, Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).

Mhandisi Hersi amesema: “Nakumbuka Aliyekuwa Kocha wetu wakati huo, Luc Eymael alitaka kuchezesha Golikipa wa wakati huo, Ramadhan Kabwili acheze nafasi ya ushambuliaji kutokana na uhaba wa Wachezaji katika Kikosi, lakini kwa sasa mnaona wenyewe maboresho makubwa yaliyofanywa kuna ushindani wa hali ya juu ndani ya timu.”

SOMA NA HII  KUHUSU KOCHA MPYA WA SIMBA..YANGA WASHINDWA KUJIZUIA...INJINIA HERSI AFUNGUKA HAYA...