Home Burudani FIFA WAANZA KUMFUATILIA DIAMOND PLATNUMZ

FIFA WAANZA KUMFUATILIA DIAMOND PLATNUMZ

 


Ukurasa rasmi wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kwa ajili ya Kombe ya Kombe la Dunia, limemfollow msanii nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Abdul Naseeb, amefuatwa na ukurasa huo ikiwa imepita mwaka mmoja tangu alipotembelea makao makuu ya shirikisho hilo.

Machi mwaka jana msanii huyo anayefanya vizuri hapa Bongo na nje ya nchi, alitembelea ofisi za Fifa zilizopo Zurich nchini Uswisi.

Katika ziara hiyo mkali huyo wa kibao cha Waah! alipokelewa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Fifa, Fatma Soumora ambapo pamoja na mambo mengine alipata wasaa wa kuhushudia kwa macho kombe la dunia.

Pia alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo kikombe kidogo na jezi iliyoandikwa jina la Platnumz 9 mgongoni na kupata chakula cha mchana akiwa  sambamba na uongozi mzima wa WCB.

SOMA NA HII  MWAKINYO: KUWA NAMBA MOJA AFRIKA NI DENI KWANGU