Home Burudani MWAKINYO: KUWA NAMBA MOJA AFRIKA NI DENI KWANGU

MWAKINYO: KUWA NAMBA MOJA AFRIKA NI DENI KWANGU


BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefunguka kuwa kutajwa kama bondia namba moja kwa viwango vya ubora Afrika uzito wa Super Welter, ni deni kubwa sana kwake kuona anajituma kufanya vizuri zaidi.

Mwakinyo kupitia mtandao unaotunza takwimu za mabondia duniani ametajwa wa Boxrec ametajwa kuwa namba moja Afrika, na namba 37 Duniani kati ya Mabondia 2,050 kwenye uzani wa Super Welter.

Akizungumzia mafanikio hayo Mwakinyo amesema: “Namshukuru Mungu, na sapoti ya Watanzania wote bila kusahau uongozi wangu. Naamini kuwa namba moja Afrika sio kitu kidogo, hivyo nina deni kubwa la kuendelea kupambana kuongeza ubora wangu.”

Mabondia wengine wa Tanzania waliotajwa kwenye listi hiyo ni Kulwa Bushiri nafasi 21, na Nicholaus Michael Mdoe nafasi ya 22.

SOMA NA HII  UMEWAHI KUOTA NDOTO BORA? HII INAKUHUSU KUTOKA KASINO YA MERIDIANBET....!