Martinez
Habari za michezo

ATUMIA MIL 56 KUNUNUA MBWA WA KULINDA MEDALI ZAKE ZA KOMBE LA DUNIA…

admin January 2, 2023 8:52 pm

Mlinda mlango wa Argentina na Aston Villa, Emiliano Martinez amemnunua Mbwa kwa kiasi cha pauni 20,000 (sawa na takribani Tsh milioni 56) kwa ajili ya kulinda nyumba na medali zake za kombe la Dunia zilizopo nyumbani kwake huko England.

Mbwa huyo ni aina ya Belgian Shepherd Malinois waliopitia mafunzo kwa ajili ya vikosi maalum.

Martinez alikuwa na kiwango bora kwenye fainal za kombe la dunia nchini Qatar, ambapo alifanikiwa kuiwezesha Argentina kushinda mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa.

Katika michuano hiyo, ambayo pia Martinez aliibuka golikipa bora wa mashindano, alipata umaarufu kwa kuokoa mikwaju ya penati katika hatua ya Robo Fainal na fainal.

Aidha, alimaliza michuano hiyo kwa kuacha kituko uwanjani ambapo wakati anakabidhiwa tuzo yake ya golikipa bora, alifanya ishara isiyo ya kiungwana , ambapo baadaye alikuja kuitolea maana , akisema kuwa ilikuwa ni ‘dongo’ kwa wafaransa.

MZEE WA KUWAJAZA ANUKIA COASTAL UNION…YANGA SC WAANIKA DILI LILILOKATALIWA… MGUNDA AMTISHA KOCHA MPYA SIMBA SC…DIARRA NA YANGA SC KAMA MLIVYOSIKIA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply