Home Habari za michezo YANGA SC WAPELEKA KIKOSI CHA ‘YANGA B’ KWENYE MAPINDUZI CUP….

YANGA SC WAPELEKA KIKOSI CHA ‘YANGA B’ KWENYE MAPINDUZI CUP….

Yanga SC B

Wachezaji 25 wa kikosi cha Yanga SC wamewasili tayari kwa ajili ya mashindano ya Mapinduzi huku mastaa wao wote wa kikosi cha kwanza wakiachwa Dar es Salaam.

Kikosi hicho kikiongozwa na Kocha msaidizi Cedrick Kaze ambaye ameongozana na mastaa wa kikosi cha kwanza nahodha Bakari Mwamnyeto na Farid Mussa kitakuwa na mchezo kesho kutwa dhidi ya KMKM.

Mastaa wengine wa kikosi cha Yanga SC ni Zawadi Mauya, Gael Bigirimana, Crispin Ngushi, Dickson Ambundo, Clement Mziza, David Bryson, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ Abdallah Shaibu Ninja na Kipa Erick Johora.

Wachezaji wa zamani wa Yanga SC ambao wapo kwenye mchakato wa kuingizwa kwenye usajili mpya ndani ya timu hiyo Lazarous Kambole na Yacouba Sogne ni miongoni mwa mastaa waliokuja kushiriki Mapinduzi.

Wachezaji walioongezwa kikosini kutoka timu ya vijana ni makipa Hajji Mohammed Abassi, Jacob Timoth Ipwaya, mabeki Maulid Kiakala, Ally Said Mohammed na Mohammed Omary.

Wakati viungo ni Arafat Hussein, Ahmed Fred, Maulid Timoth na eneo la ushambuliaji ni Nasri Ally, Rymond Ntaudyimara, Daruwesh Rashid na Shaibu Shaibu Mtita.

SOMA NA HII  FT: COASTAL UNION 1- 2 SIMBA SC....'KIFARU CHA KINYARWANDA' CHAIOKOA SIMBA...WAGOSI WALIBANA...