Fei toto Yanga SC
Habari za michezo

YANGA SC WASHINDWA KUJIZUIA SAKATA LA KUACHWA NA FEI TOTO….WAFUNGUA KESI ….

admin January 4, 2023 6:27 am

Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Yanga SC umewasilisha mashataka dhidi ya Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei toto’ katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Fei Toto aliyejiunga na Yanga SC Agosti 15-2018 akitokea JKU ya Zanzibar, kabla ya kutimka Kambini mkataba wake klabuni hapo ulitarajiwa kumalizika Mei 30-2024.

Chanzo cha Habari kutoka Yanga SC kinaeleza kuwa Uongozi wa Klabu hiyo kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu Andre Mtine, umewasilisha Barua ya mashtaka kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ili wamuite Fei Toto kwa ajili ya kuzungumzia sakata lake la kuondoka Kambini na kutaka kuvunja Mkataba.

“Tayari Yanga SC wameshawasilisha Barua kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF wakiomba Fei Toto aitwe ili waweze kuzungumzia sakata lake hilo la kutoroka kambini na kuomba kuvunja mkataba kinyume na utaratibu.”

“Tayari Barua imeshatumwa TFF na wamethibitisha kuipokea na kumfahamisha Fei Toto, hivyo tunaamini ndani ya juma hili ataitwa ili akajieleze nini kilichomfanya atoroke na kuvunja mkataba kinyemela.”

“Kama hatakuwa na sababu za msingi basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kuadhibiwa.” kimeeleza chanzo cha Habari kutoka Young Africans.

Desemba 23-2022 zilitoka taarifa za Fei toto kuandika Barua ya kuvunja Mkataba wake ndani ya Klabu ya Young Africans, ambapo tangu hapo hajaonekana kambini akitimkia kwao Zanzibar kabla ya hivi karibuni kusafiri kwenda Dubai kwa mapumziko.

YANGA WATAMBA UWEPO WA AZIZ KI….JEMBE JIPYA LATUA FASTA….SIMBA SC OUT…. BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA AJABU…MGUNDA AIBUKA NA HILI KUHUSU MZAMIRU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply