Mzamiru akiwajibika Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA AJABU…MGUNDA AIBUKA NA HILI KUHUSU MZAMIRU…

admin January 4, 2023 6:29 am

Kiungo wa Simba SC, Mzamiru Yassin ameonekana kuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni na kuisaidia timu kucheza vizuri jambo lililomuibua kocha wake Juma Mgunda na kufichua siri ya ubora huo.

Mzamiru amekuwa moja ya wachezaji wenye namba ya uhakika ndani ya kikosi cha Simba SC tangu ameingia Mgunda mwanzoni mwa msimu huu na kuwaweka nje viungo wengine wanaocheza eneo lake wakiwemo, Jonas Mkude, Victor Akpan, Nassor Kapama na Nelson Okwa na hapa Mgunda anafunguka siri ya mafanikio hayo.

“Mzamiru ni mchezaji mzuri sana. Anajua nini afanye akiwa ndani ya uwanja kwa kufuata maelekezo na anaelewana vizuri na wenzake,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Sifa nyingine ya kipekee kwa Mzamiru anaweza kukaba na kuchezesha pia ana pumzi na nguvu kubwa na nilivyofika nilimwambia anahitaji kuonyesha alichonacho na kucheza kwa kujiamini zaidi ndio maana kwa sasa unamuona kwenye ubora huo.”

Mzamiru amekuwa akicheza kama kiungo namba nane na amepangwa na Sadio Kanoute katika eneo la kati na muunganiko wao umeonekana kuwa bora zaidi na kuziunganisha vyema safu za ulinzi, kiungo na ushambuliaji za Simba. Hadi sasa Mzamiru yupo kwenye orodha ya mastaa watano wa juu wanaoongoza kwa kutoa pasi za mabao ‘Asisti’, akiwa nazo tano nyuma ya Clatous.

YANGA SC WASHINDWA KUJIZUIA SAKATA LA KUACHWA NA FEI TOTO….WAFUNGUA KESI …. HAKIKISHA MKEKA WAKO UNASOMA ODDS HIZI ZA KIBABE KUTOKA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply