Habari za Yanga SC
Habari za michezo

ACHANA NA MUDATHIR…..VYUMA HIVI NAVYO KUTUA YANGA SC WAKATI WOWOTE…

admin January 6, 2023 7:18 am

Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kuwa baada ya kufanikisha usajili wa Mudathir Yahya na kutambulishwa rasmi, bado kuna mashine nyingine watazitambulisha hivi karibuni mara baada ya kukamilisha usajili wao.

Yanga SC juzi Jumamne walimtambulisha aliyekuwa kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya ambaye tayari ameshajiunga na timu ya Yanga ambayo inashiriki michuano ya Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe alisema kuwa mara baada ya kumtambulisha mchezaji huyo bado watafanya usajili wa wachezaji wengine na kuwatambulisha kwani bado hawajamaliza usajili wao katika dirisha hili huku akitamba kuwa utakuwa usajili wa maana.

“Ni kweli tayari tumeshamtambulisha Mudathir lakini bado hatujamaliza kwenye suala la usajili kwani tutafanya usajili mwingine wa maana kupitia dirisha hili dogo na tutawatambulisha hivi karibuni vifaa vyetu.

“Usajili tutakaoufanya utakuwa ni funga kazi hivyo watu wanatakiwa kuwa watulivu kwani hatujamaliza na tutawafurahisha kama kawaida yetu,” alisema kiongozi huyo.

ISHU YA MANZOKI NA SIMBA SC….IMEBAKI HIVII TUU YANI….JAMBO LINAENDA KIMYA KIMYA…. HAJI MWINYI.: YANGA SC BADO HAIJAPATA BEKI KAMA MIMI….WALINIFANYA NIKAPOTEZA ‘DEMU’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply