Habari za Yanga SC
Habari za michezo

SAKATA LA FEI TOTO….YANGA SC WANAONGOZA 1-0….HUKUMU KAMILI KUJULIKANA JUMATATU…

admin January 7, 2023 7:18 pm

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeamua kuwa kiungo Feisal Saluma Abdallah (Fei Toto) bado ni mchezaji wa klabu ya Yanga SC kwa mujibu wa Mkataba.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 7 Januari, 2023 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo imesema uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri utatolewa Jumatatu tarehe 9 Januari, 2023.

Feisal Salum alituma barua Yanga SC mwishoni mwa mwaka jana akiomba kuvunja mkataba na kalabu ya Yanga na tangu wakati huo hajacheza mchezo wowote wala kufanya mazoezi na kikosi cha Yanga.

Kufuatia sakata hilo Yanga SC waliandika barua TFF, wakidai utaratibu haukufuatwa wakati mchezaji huyo alipoomba kuvunja mkataba.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana Januari 6,ambayo pande zote (Yanga na Feisal Salum) ziliwakilishwa na wanasheria wao katika ofisi za TFF.

Habari za Yanga leo

ILE ISHU YA YANGA KUMSAJILI ULIMWENGU…UKWELI UKO HIVI….BOSI AANIKA MCHORO WOTE… ACHANA NA SAIDOO…CHUMA HIKI KINGINE CHA MAANA KUTUA SIMBA SC…MBRAZILI KAMPITISHA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply