YANGA imetupwa nje katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars ambayo imeifanya timu hiyo kukusanya pointi nne sawa na Yanga wakitofautiana mabao ya kufunga sasa wanaenda kuvaana na Azam FC hatua ya nusu fainali.
Singida imebebwa na ushindi wake wa kwanza dhidi ya KMKM ikishinda mabao 2-0 wakati Yanga walishinda bao 1-0 wanapointi nne na mabao mawili.
Mchezo ulikuwa bora kwa pande zote mbili huku Singida Big Stars ikionekana kuwa imara zaidi eneo la kiungo ambao waliwazidi Mudathil Yahya na Zawadi Mauya wa Yanga.
Kwenye mchezo huo Singida ndio walianza kufunga dakika ya 22 kupitia kwa Fancy Kazadi bao ambalo lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika.
Bao la Kazadi liliwaamsha Yanga ambao walicheza mpira wakionyesha kuhitaji kusawazisha na dakika ya 63 David Bryson aliisawazishia timu yake bao la mpira wa kutenga ambao aliichonga moja kwa moja hadi kwenye nyavu.
Mabao hayo yalidumu hadi dakika tisini za mchezo zilipoisha na kiungo Said Ndemla ambaye alikuwa na mchezo mzuri aliibuka mchezaji bora wa mechi huku Mudathil wa Yanga akiibuka mchezaji bora mwenye mchezo wa kiungwana.
mimi nadhani msipotumia peni yenu na taaluma kueleza ukweli mtabaki na habari mipasho mpaka mwisho wa dunia.ok zote zimetolewa lkn yanga imeonyesha uwezo mkubwa lazima ligi kuu watu wajipange nakwmabi…wacha unazi simba yanga hazipo renk moja yanga ipo juuuu saana