Tetesi za Usajili Yanga
Habari za michezo

WAKILI;- FEI TOTO HANA MAHABA TENA NA YANGA….LABDA APEWE MTAALAMU…

admin January 9, 2023 4:14 pm

Wakili msomi Nduruma Majembe amebainisha msimamo wa mchezaji Faisal Salum juu ya sakata lake na waajiri wake, Yanga SC na kueleza kuwa nyota huyo hana tena mahaba ya kurudi na kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Fei Tato alihojiwa na wajumbe wa kamati aliweka dhahiri kwamba hakuna uwezekano na hawezi tena kurudi kuichezea ile klabu.

“Mchezaji ameshasema hana mahaba na timu na hawezi kuitumikia” Nduruma Majembe wakili wa Fei Toto akizungumza kupitia #tbctaifa

Majembe ameongeza kuwa Uamuzi wa Kamati kutoa hukumu kuwa Feitoto arejee kuendelea kuitumikia klabu hiyo ni kitu kigumu kwa Feitoto na kubainisha kwamba labda kama atapatiwa msaada wa kisaikolojia wa kumwezesha kutamani kurudi.

USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA HUU HAPA….ALIKUWA ANAKIPIGA ZNZ…. BAADA YA MUDATHIR YAHAYA…JEMBE LINGINE LINALOTUA YANGA HILI HAPA….NABI ABARIKI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply