Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ amewashukuru wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wanaomaliza muda wao na amewatakia heri wanachama kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 29.
“Namshukuru Afisa Mtendaj Mkuu wetu, Barbara Gonzalez kwa kazi nzuri aliyoifanya naaamini ataendelea kuwa Simba na sisi tutaendelea kumpa ushirikiano,” amesema Mo.
Mwisho kabisa Mo amewataka wachezaji kutosikiliza maneno ya watu kuhusu yeye na kwani bado yupo sana na anawapenda na anaipenda mno Simba.
Mo ameyasema hayo akiwa na timu ya @simbasctanzania ambayo imekita kambi ya wiki moja kwaajili ya mashindano mbalimbali.