Habari za Yanga
Habari za michezo

SAKATA LA FEI TOTO…YANGA WAAMUA KAMA ‘MBWAI NA IWE MBWAI’…WAMPIGA BEI….

admin January 13, 2023 7:02 pm

Uongozi wa Yanga, umeweka bayana kuwa, wapo tayari kumuuza kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na mchezaji mwingine yeyote kwenye timu hiyo kama tu utaratibu utafuatwa kwa pande zote.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema, watu wamekuwa wakizungumza tofauti kwenye sakata la Fei Toto na kubwa ikiwa ni kuwasema viongozi kuwa huwa hawapendi kuwaachia wachezaji waondoke wanapotakiwa na timu zingine.

Akizungumza, Kamwe alisema: “Yanga ni timu ya biashara, kwa hiyo haiwezi kukataa kumuuza mchezaji yeyote kama utaratibu utafuatwa. Tatizo kubwa ni utaratibu tu.

“Tunaweza kumuuza Fei Toto na mchezaji mwingine yeyote kama utaratibu utafutwa, sisi hatukukataa kumuuza, ilitakiwa kuwe na mazingira yanayotakiwa.”

DILI LA MAKUSU KUTUA SIMBA LAFIKIA PATAMU…VIFAA VINGINE HIVI HAPA …. WAKATI MBRAZILI AKIANZA MAMBO SIMBA…MO DEWJI KAMTAZAMA WEE..KISHA AKAMTAJA MGUNDA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply