Home news KABLA YA DIRISHA KUFUNGWA LEO….CHUMA HIKI KINATUA SIMBA KUUNGANA NA CHAMA…

KABLA YA DIRISHA KUFUNGWA LEO….CHUMA HIKI KINATUA SIMBA KUUNGANA NA CHAMA…

Habari za Simba

Kabla au baada ya mechi ya Arsenal na Spurs Jumapili, mashabiki wa Simba watakuwa wenye furaha sana. Kocha, Oliveira Robertinho atatangaza mashine mbili mpya kwenye nafasi tofauti kabla dirisha halijafungwa.

Simba kabla ya dirisha dogo halijafungwa leo Jumapili usiku, watashusha vyuma viwili akiwemo kiungo Mburkinabe, Ismael Sawadogo ambaye ametangazwa jana akitokea  Difaa El Jadida timu ya zamani ya Mtanzania Saimon Msuva iliyopo Ligi Kuu ya Morocco.

Robertinho baada ya kuanza kazi mapendekezo ya kwanza ilikuwa kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kuzuia na kushambulia walikubaliana kumfuatilia na kuona uwezekano wa kumpata, Banfa Sylla anayecheza Maghreb de Fes ya Morocco.

Huyu uwezekano wa kumpata ni finyu kwani mkwanja unaotakiwa ni mrefu sana ili kuvunja mkataba wake pamoja na maslahi ya mchezaji.

Mabosi wa Simba wakapiga chini dili hilo na jana mchana wakati wanapiga pilau mchana wakakubaliana kumsajili, Sawadogo ambaye kwa sasa ni mchezaji huru. Kama mambo hayatakwenda tofauti Sawadogo atachukua nafasi ya Victor Akpan ambaye atatolewa kwa mkopo licha ya mwenyewe kupinga maamuzi hayo akiamini anao uwezo wa kushindania nafasi ya kucheza Msimbazi.

Chuma kingine ambacho Simba itakitambulisha kama mambo hayatakwenda tofauti ni straika Mkongomani,Juan Makusu ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunjiwa mkataba na FC Lupopo ya DR Congo.

Awali mabosi wa Simba walitaka kumnunua straika wa TP Mazembe Juan Baleke lakini Mazembe wakaweka ngumu wakitaka kumuachia kwa mkopo, jambo ambalo lilizua mvutano Simba mpaka walipoamua kuendelea na Makusu ambaye sasa atatua Msimbazi.

Inafahamika kwamba licha ya mvutano baadhi wakihofia uwezo wake, tayari Makusu ametumiwa mkataba akiwa na DR Congo inayojiandaa na mashindano ya CHAN yanayoanza leo nchini Algeria.

Baada ya Makusu kumaliza CHAN, atawasili nchini kuanza kazi Simba na atachukua nafasi ya Nelson Okwa aliyekubali kutolewa kwa mkopo kwenye timu yoyote yenye mazingira mazuri hapa Tanzania.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ jana aliwasili Dubai kuongeza nguvu kwenye kambi ya timu hiyo ikiwemo kushuhudia mechi mbili za kirafiki na kukamilisha masuala hayo ya usajili nchini Algeria.

Try Again alisisitiza dirisha hili la usajili wanalitumia vizuri kujaza mapengo yaliyopo na kutimiza hitaji la kocha Mbrazil Oliveira Roberto la kuhitaji mshambuliaji wa kusaidiana na waliopo.

“Tunafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi na hiyo ndiyo kazi yetu viongozi hivyo mashabiki na wanachama wa Simba wenyewe waendelee kutuamini,”alisema Try Again.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...AZAM FC NAO HAWAKO NYUMA AISEE...WAMNYATIA BEKI KISIKI WA YANGA....