Klabu ya Simba imemtambulisha mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Jean Othos Baleke kutoka TP Mazembe kwa mkataba wa miaka miwili hadi 2025.
Mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kwa staili zote, anakuja Simba huku akitumainiwa kuwa tiba ya tatizo la muda mrefu katika safu ya ushambuliaji.
Kusajiliwa kw Baleke, ni sehemu ya mkakati wa makusudi wa kocha Mbrazili Robertinho katika kukisuka kikosi hiko ambacho siku anakabidhiwa alihaidi kukifikisha Fainal ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Baleke anakuja Simba ikiwa ni mara baada ya kushindikana kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Vipers Manzoki ambaye hivi sasa anacheza soka la kulipwa nchini China.
Kwa muda mrefu Simba walikuwa wakihaha kutafuta mshambuliaji wa kati mara badaa ya Mserbia Dejan kuondoka mwanzoni mwa msimu huu kwa kile alichodai kushindwa kutimiziwa mahitaji yake.
Hata hivyo, Dejan alisajiliwa kwa lengo la kuzinba nafasi ya Medie Kagere ambaye aliachwa mwanzoni mwa msimu huu.
Baleke anajiunga na Simba ambayo hivi sasa wanasafu imara ya ushambuliaji kwa mujibu wa takwimu za Ligi kuu, kwani mpaka sasa washambulaiji wao, Moses Phiri, John Bocco , Saidoo Ntibazoniza na wengineo wanaocheza mbele wamefunga zaidi ya magoli 30 kitu ambacho kinaonyesha kuwa sio butu sana kulingana na hofu ya mashabiki ilivyo.
Moja ya jukumu au mtihani mkubwa wa Baleke ndani ya Simba ni kupigania namba mbele ya washambuliaji hao, lakini pia kushirikiana na wenzake kuipeleka Simba kwenye hatua za juu zaidi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrik.
Aidha katika upande mwingine, Chanzo chetu cha habari ndani ya klabu ya Simba kimefichua kuwa, Baleka atalipwa mshahara wa Dola 5500 sawa na zaidi ya milioni 12 za kitanzania, huku akipewa bonasi ya usajili ya dola 60000 zaidi ya milioni 120 za kitanzania.
Mbali na hayo, Baleka atapewa nyuma ya kisasa pamoja na usafiri atakotumia akiwa hapa Tanzania, pia kwenye mkataba wake kuna kipengele cha kuuzwa endapo atapata timu kubwa zaidi Afrika au Ulaya.