Home Habari za michezo BAADA YA KUUBONDA JANA…MUDATHIR YAHYA AWASHIWA TAA YA KIJANI YANGA…NABI ASHINDWA KUJIZUIA…

BAADA YA KUUBONDA JANA…MUDATHIR YAHYA AWASHIWA TAA YA KIJANI YANGA…NABI ASHINDWA KUJIZUIA…

Habari za Yanga

Kocha wa Mkuu wa Yanga Nasreddine Mohammed Nabi amefurahi na kuwapongeza viongozi wa klabu hiyo, kwa kufanikisha usajili wa kiungo kutoka Zanzibar Mudathir Yahya, ambaye amekiri alikuwa anamuhitaji kwa udi na uvumba.

Mudathir Yahya amesajiliwa Yanga akiwa mchezaji huru wakati wa Dirisha Dogo la Usajili lililofungwa rasmi juzi Jumapili (Januari 15).

Kocha Nabi amesema Kiungo huyo wa zamani wa Azam FC, ana uwezo mkubwa ambao anaamini utakisaidia sana kikosi chake katika harakati za kutetea Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, pamoja na kufanya vizuri Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi.

“Nimefurahi na nawapongeza viongozi wa Yanga kwa kufanikisha usajili huu. Mudathir nilimuhitaji kwenye kikoso changu tangu msimu uliopita lakini haikuwa rahisi kumpata, ujio wake nimeufurahia.”

Akizungumzia kiwango alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Ihefu FC Nabi amesema Mudathir amecheza kwa asilimia 50% ya vile anavyotaka acheze hivyo anaamini ataendelea kuimarika na atakapofikia asilimia 100% Mashabiki wa Yanga watafurahi.

“Ninaamini bado hajaonesha uwezo wake kwa asilimia 100, amecheza vizuri dhidi ya Ihefu FC na mchango wake umeonekana kwa asilimia 50, ninaamini kuna siku mashabiki watafurahi zaidi ya leo (jana).” amesema Nabi

Mbali na Mudathir, wengine waliosajiliwa Yanga wakati wa Dirisha Dogo ni Mlinda Lango Metacha Mnata, Beki Mamadou Doumbia (Mali) pamoja na Mshambuliaji Kennedy Musonda (Zambia).

SOMA NA HII  KUHUSU USAJILI WA CHAMA..SIMBA WATOA TAARIFA MPYA...AHMED ALLY AFICHUA 'CODE'...