Habari za michezo
ISHU YA MASTAA WAPYA SIMBA…AHMED ALLY ATOA RATIBA MPYA YA MASHABIKI KUWAONA…
admin
January 18, 2023
8:17 am
Meneja wa Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mchezaji Jean Beleke atawasili leo nchini na baada ya hapo ataelekea Uwanja wa Mkapa kusalimiana na mashabiki wa timu hiyo lakini hatocheza mchezo dhidi ya Mbeya City.
Beleke ni mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba akitokea Nejmeh ya Lebanon kwa mkopo, aliwahi kuitumikia TP Mazembe ya DR Congo.
Akizunguma hii jana mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally amesema ujio wa mchezaji hao utaambana na wa Sawadogo Ismaël ambaye atakuwepo kwa ajili ya kusalimia na mashabiki kuangalia mchezo huo.
“Kama atawasili mapema (Jean Beleke) naye ataelekea uwanjani kusamilia mashabiki, usajali huu unaenda kutibu matatizo tuliyokuwa nayo ni wachezaji mahususi kwa ajli ya maeneo yaliyolega.” amesema Ahmed.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.