Habari za Simba SC
Habari za michezo

WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKILIA NA ‘SUB’ YA CHAMA…MBRAZILI KAWASIKIA..KISHA AKAJIBU HIVI..

admin January 19, 2023 8:04 pm

Kocha Mkuu Klabu ya Simba SC,Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema ushindi wa mabao 3-2 ambao Simba iliupata hapo jana dhidi ya Mbeya City ni jambo la kwanza alilokuwa anahitaji na limemfanya afurahi.

Robertinho amesema amefurahishwa na wachezaji walivyocheza kitimu licha ya kuwa amekaa nao kwa muda mfupi.

“Ilihitajika ushindi bila kujali tumechezaje, tupo kwenye mbio za ubingwa tunapaswa kushinda kila mchezo hasa tukiwa nyumbani.

“Ndiyo kwanza nina siku nane tangu nilipoanza kazi. Simba ni timu kubwa na malengo yake ni makubwa pia kama nilivyo mimi”

“Jambo jengine lililonifurahisha ni jinsi tulivyocheza, wachezaji walicheza kitimu ingawa kulikuwa na makosa kadhaa ambayo tunapaswa kuyaondoa.

“Nimeanza kupata mwanga wa kikosi ambavyo kinapaswa kiwe,” amesema Robertinho.

HIZI HAPA SABABU YA KIFO CHA MCHEZAJI WA U17 WA SINGIDA BIG STAR ALIYEFIA UWANJANI LEO.. KUBALI AU KATAA…ILA KITAKWIMU…NTIBAZONKIZA KAZIDIWA NA MAYELE TU YANGA NZIMA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply