Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI ‘WAKIENJOY’….KUMBE NABI ‘KAVURUGWA’ NA USAJILI WA MUSONDA YANGA…

WAKATI MASHABIKI ‘WAKIENJOY’….KUMBE NABI ‘KAVURUGWA’ NA USAJILI WA MUSONDA YANGA…

Habari za Yanga

Usajili wa dirisha dogo umewapa jeuri mashabiki wa Yanga wakiwatambia Simba, kuwa kuna siku makocha wao ikiwapendeza wanaweza kupanga mziki wa wachezaji wazawa pekee na bado watu wataumia.

Hapo hapo wakaongeza, ipo siku kuna mziki wa wageni pekee utashushwa na watu wakakimbiana, lakini kocha Nasreddine Nabi akakakazia akisema kwa sasa kama kuna kitu kinampa presha ni jinsi ya kuipanga timu hiyo, hasa kutokana na ingizo la Kennedy Musonda na uwepo wa Fiston Mayele.

Mayele ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo akifunga 15, akiwa ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara, huku Musonda akitua kikosini akitoka kuwa kinara wa mabao wa Ligi Kuu Zambia akifunga 11 katika mechi 17, akimuacha anayemfuata nyuma yake kwa mabao matano.

Hapo ni mbali na uwepo kwa Stephanie Aziz KI na nyota wengine ambao wanakimbiza kwa kufunga mabao na kuasisti katika kikosi hicho, jambo linalompa wakati mgumu Nabi wa kuamua aanze na nani kulingana na mechi anazocheza kwa sasa.

Kocha Nabi alisema katika kikosi chake alichonacho sasa presha kubwa kwake ni jinsi ya kutoa nafasi kwa kila mchezaji wa kikosi chake, hasa kwenye eneo la ushambuliaji kutokana na Musonda na Mayele kuwa kwenye ubora stahiki.

Nabi alisema kikosi chake kimekamilika vizuri ambapo kama kila mchezaji anakuwa na afya njema kuna kazi nzito ya kugawanya nafasi. Hata hivyo, Nabi amewapa akili wachezaji wake akiwaambia kama kuna mtu yuko fiti basi njia rahisi ni kushindana kwa akili kubwa kuanzia mazoezini kwani hatosumbua akili yake kama kuna mchezaji hatajituma kwenye uwanja wa mazoezi au hata kwenye mechi.

“Ni timu bora kabisa tuliyonayo, kuwa na kundi la wachezaji bora kama hawa ni presha kubwa kwetu kama kocha kuhakikisha kila mchezaji anayekuwa na afya njema na yuko fiti kuhakikisha anacheza,” alisema Nabi.

“Nawapongeza sana viongozi kuanza na mfadhili wetu Ghalib Said na rais wetu na viongozi wenzake kwa kuunda timu kama hii ambayo kwanza ni gharama kubwa kupata watu bora kama hawa na kuwatunza, naona mambo mengi sio kitu rahisi.

“Kila mchezaji sasa anatakiwa kujiandaa kutoa mchango wake, tuna mechi nyingi za mashindano, ukiangalia tuna mechi zisizopungua 21 katika mashindano yote kila mchezaji anatakiwa kuongeza ushindani kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi.

“Upo mchanganyiko mabao unaweza kuugawanya kupata timu ambayo itakwenda kushindana, hata hiyo ya wazawa na wageni inawezekana lakini hatutaki kwenda huko kama makocha, tunachotakiwa ni kuchagua timu imara ambayo itakwenda kupigania ushindi wa Yanga.”

Mziki ulivyo Ukianza na kikosi cha wazawa pekee Yanga inaweza kutengeneza kikosi cha wazawa pekee kisha wakatengeneza timu ya ushindani na ikatoa ushindi.

Kikosi cha wazawa kinaweza kuwahusisha kipa Metacha Mnata langoni mabeki wakiwa Kibwana Shomari, David Bryson, nahodha mkuu Bakari Mwamnyeto na Dickson Job.

Safu ya kiungo ikiundwa na Zawadi Mauya, Mudathir Yahya, Dickson Ambundo, Salum Aboubakar ‘Sure boy’, Farid Mussa na mshambuliaji Clement Mzize huku wa akiba wakiwa Erick Johora, Ibrahim Bacca, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Crispin Ngushi, Denis Nkane na Feisal Salum.

Mziki wa wageni ni huu

Sura nyingine Yanga inaweza kuwa na mziki wa wageni pekee na mmoja akabaki nje ambapo langoni atakuwa kipa Djigui Diarra, Djuma Shaban,Joyce Lomalisa, Yannick Bangala na Mamadou Doumbia.

Safu ya kiungo ikiwa na Khalid Aucho, Stephane Aziz KI, Jesus Moloko, Bernard Morrison huku washambuliaji wakiwa Fiston Mayele, Kennedy Musonda wakati winga Tuisila Kisinda akianzia benchi.

Kikosi wazawa Metacha Kibwana Bryson Mwamnyeto Job Mudathir Mauya Ambundo Sure boy Mzize Farid

Sub Johora Mauya Ninja Bacca Ngushi Nkane Feisal.

Kikosi wageni Diarra Djuma Lomalisa

SOMA NA HII  HASIRA ZA CARLINHOS ZAMVURUGA KAZE YANGA