Habari za Simba
Habari za michezo

KISA SAWADOGO…MAFISANGO AKUMBUKWA SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin January 27, 2023 6:05 pm

Beki wa zamani wa Klabu za Simba SC na Young Africans, Amir Maftah, amewataka Mashabiki wa Soka Tanzania kumpa muda kiungo Ismail Sawadogo, ili kuona anafaa kufananishwa na Patrick Mutessa Mafisango.

Maftah ametoa kauli hiyo kufuatia sifa anazopewa Sawadogo aliyesajiliwa Simba SC wakati wa Usajili wa Dirisha Dogo mwezi huu (Januari), huku akicheza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Maftah amesema kiungo huyo kutoka Burkina Faso mchezaji mzuri ila bado ni mapema kuona kama atafanana kiuchezaji na Mafisango moja kwa moja.

“Nilitazama ile mechi bado kwa sasa ni ngumu kumfananisha moja kwa moja na Mafisango ingawa kwa muda mchache ameonyesha ana kitu mguuni kwake ngoja tumpe muda kidogo.”

“Kwa upande wa Mafisango yeye ulikuwa unamuona wakati wa kuzuia, katikati ya uwanja, alikuwa akienda kufunga, anakaba na anatengeneza nafasi huyu Sawadogo kuna baadhi ya vitu anendana naye japo vingine sijaona akivitumia sawa sawa,” amesema Maftah

Kabla ya kutua Simba SC Sawadogo alikua anaitumikia Difaâ El Jadida ya Morocco, iliyomsajili kutoka Enppi SC ya Misri.

Wengine waliosajiliwa Simba SC kupitia Dirisha Dogo ni Saido Ntibazonkiza (Burundi), Jean Baleke (DR Congo) na Mohamed Mussa (Zanzibar).

BANGALA NA DODOMA JIJI SASA MAMBO NI MUSWANO….KUANZA KUVAA JEZI YAO RASMI… BAADA YA CEO MPYA KUTANGAZWA JANA…BOSI MWINGINE ANAYEONGEZWA SIMBA HUYU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply