Home Habari za michezo HII HAPA ORODHA YA WASHAMBULIAJI ‘VIBOGOYO’ MSIMU HUU…STAA WA SIMBA NAYE YUMO...

HII HAPA ORODHA YA WASHAMBULIAJI ‘VIBOGOYO’ MSIMU HUU…STAA WA SIMBA NAYE YUMO 😂😂😂

Habari za Michezo, habari za Simba

Fiston Kalala Mayele ndio kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu hivi sasa akiwa ameshacheka na nyavu mara 15 katika michezo 21 ambayo imekwisha kuchezwa.

Wakati Mayele akibakisha bao moja kufikia idadi ya mabao aliyofunga msimu uliopita (16) huku, George Mpole (Geita Gold) akiwa mfungaji bora kwa mabao 17.

Hata hivyo, katika vita ya ufungaji bora ambayo washambuliaji wengi walianza msimu vyema kwa sasa wameonekana kunyosha mikono juu.

Reliants Lusajo mfungaji bora wa muda wote kwenye kikosi cha Namungo amefunga mabao sita sawa na Pape Sakho (Simba) na Feisal Salum (Yanga).

Upepo umegeuka nyota huyo kwani Namungo imecheza michezo 11 bila mshambuliaji huyo kucheka na nyavu kwani mara ya mwisho alifunga Novemba 4, walipolala 2-1 dhidi ya Mbeya City.

Hata hivyo, kocha wake, Denis Kitambi ameendelea kumtetea kwa kueleza ni mapito tu ambayo nyota huyo anayapitia na muda wowote atakuwa sawa.

“Mshambuliaji yeyote anakuwa na furaha pale anapopata nafasi ya kufunga, lakini inapokuwa tofauti inamtoa kwenye morali hivyo naamini atakaa sawa muda si mrefu,” alisema Kitambi.

Meddie Kagere (Singida) mfungaji bora mara mbili msimu wa mwaka 2018/19 kwa mabao yake 23 na 2019/20 kwa mabao 21 hadi sasa amefunga mabao matano na mara ya mwisho amefunga Disemba 17 kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Prisons na tayari imepita michezo sita bila kufunga.

Habib Kyombo (Simba) mwenye mabao mawili kwenye ligi mara ya mwisho alifunga Oktoba 2 wakati Simba ikiichapa Dodoma Jiji mabao 3-0. Simba tayari imecheza michezo 16 tangu, Kyombo afunge.

Danny Lyanga (Geita) msimu uliopita alimaliza ligi na mabao sita, hadi sasa amefunga mabao mawili, kitu ambacho kinazidi kuwaumiza vichwa makocha hasa katika safu ya ushambuliaji. Mara ya mwisho alifunga Desemba 25 katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Kagera.

Matheo Anthon (KMC) ambaye msimu uliopita alimaliza ligi na mabao tisa hadi sasa amefunga mabao manne na mara ya mwisho akifunga Septemba 20 ikiwa michezo 17 imepita tangu alipofunga.

SOMA NA HII  TFF YAWAPIGIA MAGOTI GSM...WARUDI MEZANI UPYA KUJADILI DILI..MGUTO ATUPA MPIRA KWA KIDAO..