Mkutano Mkuu wa Simba Leo
Habari za michezo

MKUTANO MKUU WA SIMBA: MANGUNGU AJIPIGIA ‘UPATU’ KIAINA….AFUNGUKA ISHU YA PROPAGANDA…

admin January 29, 2023 2:20 pm

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, anayemaliza muda wake, Murtaza Mangungu amesema klabu hiyo iko imara na kuwataka wana Simba kutosikiliza propaganda nyingine.

Mangungu ambaye muda mfupi ujao atakuwa na kibarua cha kutetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu akipewa upinzani na Moses Kaluwa anasema wanasimba wako imara, wanaelewa na wanajua timu yao nini inafanya na zaidi wanahitaji mafanikio.

“Tusisikilize propaganda nyingine kuhusu klabu yetu,” anasema Mangungu alipohutubia mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo wenye ajenda kadhaa ikiwamo ya uchaguzi mkuu.

Bosi huyo wa Simba pia aliwashukuru viongozi kadhaa waliowahi kuongoza klabu hiyo akiwamo Ismail Aden Rage, Hasanoo na Mwina Kaduguda ambaye pia ni mjumbe wa bodi anayemaliza muda wake.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Mangungu aliwaomba wanachama wa Simba kuwaombea wenzao waliotangulia mbele ya haki.

KUTOKA MKUTANO MKUU SIMBA: CEO MPYA AMRUDISHA KUNDINI BARBARA…AFUNGUKA KIKAO NAYE… UCHAGUZI MKUU SIMBA: MANGUNGU ABADILI UPEPO …KALUWA APIGIWA YOWE UKUMBI MZIMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply