Mkutano Mkuu Simba
Habari za michezo

UCHAGUZI MKUU SIMBA: WAPIGA KURA WAGOMA….KAMATI YAINGIA ‘CHOBINGO’…

admin January 29, 2023 5:56 pm

Wapiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Simba wamegomea uamuzi wa kamati ya Uchaguzi wakati wa kuchagua wajumbe.

Kamati hiyo ambayo imeenda kujipanga, ilipofika saa 9.45 mchana ilitoa tamko la kupiga kura kwa mjumbe mmoja kati ya 12 wanaowania nafasi tano, moja ikiwa mwanamke.

Tangazo la kamati limetaka kila mpiga kura kuchagua mjumbe mmoja tu, kisha baadae atakayekuwa na kura nyingi ndiye atakuwa mshindi.

Tangazo hilo liliibua zomea zomea ukumbi mzima wapiga kura wakipaza sauti kuwa hawataki.

Katiba inaruhusu kuchagua wajumbe watano, kwanini tuchague mmoja, hatutaki, ilikuwa ni kauli za wanachama ndani ya ukumbi huo.

Kamati imekwenda chemba kujadiliana upya jambo hilo lililokataliwa na wapiga kura hao

KISA JAMBO LA FEI TOTO NA YANGA…SERIKALI WAIBUKA NA KAULI HII YA ‘KIBABE’…ISHU YA UMRI YATAJWA.. MKUTANO MKUU WA SIMBA :KAJULA AWEKA PEMBENI U-CEO WAKE…AJIPA CHEO KIPYA MBELE YA TRY AGAIN..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply