Home Habari za michezo BAADA YA KUMTAZAMA KIBU KWA SAA KADHAA…MBRAZILI SIMBA KAFANYA MAAMUZI HAYA MAPYA..

BAADA YA KUMTAZAMA KIBU KWA SAA KADHAA…MBRAZILI SIMBA KAFANYA MAAMUZI HAYA MAPYA..

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ amefunguka kwa nini aliamua kumpa zawadi Mshambuliaji Kibu Dennis, baada ya mazoezi ya juzi Jumatano (Januari 11).

Kibu Dennis amekua sehemu ya Wachezaji ambao walishindwa kukubalika kirahisi kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC msimu huu, kufuatia kuonesha kiwango cha kawaida kila alipopewa nafasi.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema: “Tukiwa kambini huwa tunafanya kazi kubwa na nzito, kwa hiyo inapotokea mchezaji anafanya vizuri, unapaswa kumpongeza kwa kumpa zawadi, ndivyo nilivyofanya mimi.”

“Zawadi ile nimeinunua mimi kama Kocha, na lengo langu ni kuendelea kuongoeza hamasa kwa wachezaji wangu wote ili wajitume kuanzia mazoezini hadi kwenye Michezo itakayotukabili.”

“Ninahitaji kuona tukicheza soka la ushindani na kila mchezaji awe na kiu ya kufanya vuzuri kila ninapompa nafasi, kwa hiyo nitaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji ili waongeze bidii ya kujituma maozezini na kwenye michezo ya ushindani ili kupata matokeo mazuri.” amesema Robertinho

Simba SC imeweka kambi Dubai-Falme za Kiarabu ikijiandaa na Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

SOMA NA HII  CHEZA KIBINGWA NA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET....!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here