Home Habari za michezo BAADA YA KUWA MAJERUHI ….PETER BANDA ALIAMSHA SIMBA…AANZA MDOGO MDOGO KUDAI…

BAADA YA KUWA MAJERUHI ….PETER BANDA ALIAMSHA SIMBA…AANZA MDOGO MDOGO KUDAI…

Habari za Simba

Nyota wa Simba, Peter Banda anaendelea na programu maalumu itakayomrejesha kwenye ubora wake hali unayoweza kuitafsiri kama kuanza kudai namba yake kwenye kikosi cha kwanza kimya kimya.

Mchezaji huyo hajaonekana uwanjani tangu mwishoni mwa mwaka 2022 baada ya kupata kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ni kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars alipata maumivu alipoingia akitokea benchi na alifunga bao moja.

Ngoma ilikuwa nzito katika mchezo huo kwa kuwa waligawana pointi moja moja kwa kufungana bao 1-1.

Banda yupo Dubai na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Robertinho Oliviera, raia wa Brazil akishirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.

Mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Novemba 9, 2022 katika mchezo dhidi ya Singida Bog Stars.

Toka asajiliwe na Simba Msimu uliopita, Peter Banda amekuwa na kiwango cha kushuka na kupanda tofauti na vile ilivyotarajiwa na wengi kuwa angekuwa mbadala wa Luis Miquissone.

Itakumbukwa kuwa Nyota huyo anayelipwa zaidi ya milioni 9 za kitanzania, alisajiliwa mara baada ya kuonyesah uwezo mkubwa kwenye mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Malawi mwaka juzi kwenye uwanja wa Mkapa.

Pamoja naye alisajiliwa Duncan Nyoni ambaye yeye hakudumu na wekundu hao wa msimbazi kwani alichunjwa kweny dirisha dogo la msimu wa 2021/22.

Hata hivyo, peter Banda amekuwa na nyakati nzuri ukiacha hizo mbaya kwani kwa kiasi fulani ameisadia Simba kwenye harakati zake za kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

Simba bado wanaimani naye kuwa ipo siku nyota huyo wa timu ya taifa ya Malawi pia atarudi kweny makali yake na kulipa gharama  walizotumia kumsajili , kwani inasadikiwa alisajiliwa kwa gharama za Milioni 56 za kitanzania.

SOMA NA HII  SAMATTA: NI BAHATI MBAYA TUNAANZIA UGENINI...NIGER NAO WANAITAMAN AFCON KAMA SISI...