Home Habari za michezo BEKI HUYU AKITUA TU PALE YANGA…BAKARI MWAMNYETO HUENDA AKACHEZEA YANGA B…

BEKI HUYU AKITUA TU PALE YANGA…BAKARI MWAMNYETO HUENDA AKACHEZEA YANGA B…

Habari za Yanga

Kabla ya dirisha la usajili kufungwa Januari 15, 2023, Tetesi mbalimbali za usajili zinagonga vichwa vya habari nchini.

Mabingwa mara 28 Ligi Tanzania Bara Yanga SC, huwenda wakamsajili na kumtangaza beki, Mamadou Doumbia raia wa Mali.

Beki huyo kisiki, mrefu wa futi 6 na inchi 2 na anayependelea zaidi kutumia mguu wake wa kulia hucheza nafasi ya Centre-Back.

Doumbia kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Mali kwenye michuano ya Chan, na mekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya taifa.

Taarifa zinasema kuwa , injinia wa mipango ya usajili wa beki huyo ni golikipa wa  Mali na Yanga, Diarra ambaye ameushawishi uongozi wa benchi la ufundi klabuni hapo baada ya kuona kuna mapungufu kwenye safu yake ya ulinzi.

Toka kuanza kwa msimu huu, kiwango cha nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeti kimeshuka hali inayopeleka kutokupangwa mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Hata hivyo, mabeki wanaopangwa pia wamekuwa hawaonyeshi ufanisi mkubwa hali inayompa shida Diarra mpaka kupelekea kufungwa magoli mepesi.

Kusajiliwa kwa Doumbia kutaifanya Yanga kuachana na mmoja wa mchezaji wake mwingine wa kigeni, ambapo taarifa zinadai kuwa huenda akawa Tuisila Kisinda ambaye hajakuwa na kiwango bora toka arudi klabuni hapo akitokea Berkane ya Morocco.

Mpaka sasa imetangaza usajiliwa Kiungo Mudathiri Yahaya akitokea KMKM ya Zanzibar, pamoja na Musonde akitokea Power Dynamo ya Zambia.

SOMA NA HII  MAYELE AIBUA JAMBO NA 'FEI TOTO'..HESABU YANGA ZAGEUKA...YAMEFICHUKA UDHAMINI WA GSM...

1 COMMENT